TUSIJE TUKASAHAU: Dkt Ruto asiwe wa kuwachenga wanawake, awape ahadi za kweli uongozini

TUSIJE TUKASAHAU: Dkt Ruto asiwe wa kuwachenga wanawake, awape ahadi za kweli uongozini

MNAMO Mei 15, 2022 Naibu Rais William Ruto alimteua Mbunge wa Mathira Rigathi Gachagua kuwa mgombea mwenza wake katika kinyang’anyiro cha urais Agosti 9, 2022.

Dkt Ruto alisema kuwa Bw Gachagua ndiye aliyeibuka bora zaidi miongoni mwa wandani wake waliowasilisha maombi wakitaka wateuliwe kwa nafasi hiyo.

Lakini Naibu Rais asije akasahau kuwa mnamo Agosti 31, 2020 aliahidi kuwamba angemteua mwanamke kuwa mgombea mwenza wake.

Dkt Ruto alitoa tangazo hilo mjini Mombasa alipokuwa akisambaza sodo kwa wanawake mjini Mombasa, akieleza kuwa wanawake ni nguzo kuu nchini wanafaa kupewa nafasi sawa katika uongozi.

Lakini juzi, licha ya kwamba wawili kati ya watu sita waliotuma maombi ya kiti hicho walikuwa wanawake, Dkt Ruto hakuteua mmoja wao.

Wawili hao walikuwa Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru na Mbunge wa Kandara Alice Wahome.

Japo Dkt Ruto aliahidi kuteua wanawake 10 katika baraza lake la mawaziri, endapo atashinda urais, huenda hii ikageuka ahadi hewa sawa na ile ambayo alitoa Agosti 31, 2020.

  • Tags

You can share this post!

CHARLES WASONGA: Serikali iweke mikakati ya kuzuia mlipuko...

Raila kukita kambi katika ngome ya Mudavadi

T L