TUSIJE TUKASAHAU: IEBC haijatoa ripoti kuhusu madai ya kuwepo kwa njama ya wizi

TUSIJE TUKASAHAU: IEBC haijatoa ripoti kuhusu madai ya kuwepo kwa njama ya wizi

MNAMO Machi 4, 2022 mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Wafula Chebukati, aliwaahidi Wakenya kwamba tume hiyo ilianzisha uchunguzi kuhusu madai ya Naibu Rais William Ruto kwamba kuna njama ya wizi wa kura katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

Akiongea mjini Naivasha katika mkutano kati ya makamishna wa IEBC na wanachama wa Chama cha Wahariri Nchini (KEG) na Muungano wa Wanahabari Nchini (KUJ), Bw Chebukati, alisema baada ya uchunguzi huo tume yake ingetoa ripoti kwa umma “haraka”.

Mwenyekiti huyo alitoa ahadi hiyo baada ya wadau na Wakenya, kwa ujumla, kulalamikia madai hayo yaliyotolewa na Dkt Ruto siku chache awali akiwa ziarani nchini Amerika.

Lakini huku zikisalia siku 47 kabla ya Wakenya kuelekea debeni kuwachagua viongozi wapya, Bw Chebukati hajatoa ripoti ya uchunguzi huo, jinsi alivyoahidi.

Aidha, mwenyekiti huyo hajawaelezea Wakenya ni kwa nini tume yake haijatoa ripoti hiyo ilhali madai hayo ya wizi wa kura ni yenye uzito wa kitaifa. Hii ni kwa sababu madai hayo yalitolewa na mshikilizi wa afisi ya pili kimamlaka nchini.

  • Tags

You can share this post!

Ryan Giggs ajiuzulu kama kocha wa timu ya taifa ya Wales

CHARLES WASONGA: IEBC ifafanue masuala tata mapema kuhusu...

T L