TUSIJE TUKASAHAU: Kenya yajikokota kusaka fidia kwa familia za wahanga na waliojeruhiwa kwenye shambulio la kigaidi katika ubalozi wa Amerika

TUSIJE TUKASAHAU: Kenya yajikokota kusaka fidia kwa familia za wahanga na waliojeruhiwa kwenye shambulio la kigaidi katika ubalozi wa Amerika

MNAMO Jumapili, Agosti 7, 2022, balozi mpya wa Amerika nchini Margaret ‘Meg’ Whitman aliongoza maadhimisho ya miaka 24 tangu ubalozi wa Amerika jijini Nairobi kushambuliwa na wafuasi wa kundi la kigaidi la Al-Qaeda mnamo Agosti 7, 1998.

Jumla ya watu 231, raia wa Kenya na Amerika waliuawa na wengine wengi wakajeruhiwa katika shambulio hilo ambalo lilishtua ulimwengu.

Huku serikali ya Amerika ikiwa imekamilisha mpango wa kutoa fidia kwa waathiriwa na jamaa za raia wake waliouawa katika shambulio hilo, serikali ya Kenya imejivuta kusaka fidia kwa raia wake. Hii imewaacha waliopoteza wapendwa wao na waliopata majeraha wakiwa na machungu mioyoni mwao.

Ni kutokana na kujivuta huku kwa serikali ya Kenya ambapo mnamo Mei 20, 2020 mashirika sita yasiyo ya kiserikali (NGOs) yaliwasilisha kesi mahakama kuishinikiza serikali ifanikishe fidia kwa wahanga hao.

  • Tags

You can share this post!

Kieni: Kanini Kega akubali sauti ya wapigakura akae kando

CHARLES WASONGA: Kenya na Somalia ziimarishe vita dhidi ya...

T L