TUSIJE TUKASAHAU: Maoni ya umma kuhusu GMOs yanafaa kuzingatiwa

TUSIJE TUKASAHAU: Maoni ya umma kuhusu GMOs yanafaa kuzingatiwa

MNAMO Jumatatu Rais William Ruto aliondoa marufuku yaliyowekewa vyakula vilivyofanyiwa mabadiliko ya kisayansi, almaarufu, (GMOs).

Taarifa kutoka Ikulu ya Rais ilisema kuwa uamuzi huo ulifikiwa kwenye kikao cha baraza la mawaziri, kufuatia mapendekezo ya jopokazi lililochunguza usalama wa GMOs na usalama wa chakula.

“Baraza la mawaziri limebatilisha uamuzi wake wa Novemba 8, 2012 uliopiga mafuruku ukuzaji wa mimea iliyofanyiwa mabadiliko ya kisayansi na uagizaji wa vyakula na lishe ya mifugo iliyozalishwa kisayansi. Kwa misingi ya hatua hii ukuzaji na uagizaji wa mahindi ya GMO sasa unaruhusiwa,” ikasema taarifa hiyo.

Lakini Rais Ruto asije akasahau kuwa uamuzi kama huo wa kisera unafaa kufanywa baada ya kushirikishwa kwa maoni kutoka kwa raia, kulingana na hitaji la kipengele cha 118 cha Katiba.

Hii ndio maana juzi aliteua jopo-kazi la kuchunguza changamoto zinazokumba utekelezaji wa mtaala wa masomo wa umilisi na utendaji (CBC).

Aidha, hii ndio maana Dkt Ruto mwenyewe ameamua Tume ya Utumishi wa Umma (PSC) kukusanya maoni kutoka kwa umma kuhusu wazo la kuteuliwa kwa Mawaziri Wasaidizi (CAS).

You can share this post!

Wakazi walalama kuhusu ongezeko la noti feki za elfu

Wabunge wamtaka Rais apunguze gharama

T L