TUSIJE TUKASAHAU: Martha Koome asije akasahau George Odunga na majaji wenzake watano bado hawajaapishwa

TUSIJE TUKASAHAU: Martha Koome asije akasahau George Odunga na majaji wenzake watano bado hawajaapishwa

JAJI Mkuu Martha Koome Ijumaa alisema kuwa Tume ya Huduma za Mahakama (JSC) itahakikisha kuwa maamuzi ya majaji na mahakimu yanaheshimiwa na kutekelezwa na asasi zote nchini.

Akiongea katika hafla fupi ya uzinduzi wa Mpango wa Kimkakati wa JSC wa 2022 hadi 2027, Jaji Koome, ambaye ni Rais wa JSC, alisema atahakikisha kuwa hilo limefikiwa kupitia mazungumzo kati yake na serikali.

Lakini Bi Koome asije akasahau kuwa mnamo Juni 2021 Rais Uhuru Kenyatta alikaidi maamuzi ya majaji wa mahakama kuu na mahakama ya rufaa kwa kukataa kuteua majaji sita kati ya 40 walioidhinishwa na JSC.

Akumbuke kuwa ahadi aliyotoa, Ijumaa, ni sawa ile aliyotoa alipokuwa akipigwa msasa kwa wadhifa huo Aprili 2021, hajaitekeleza kwa sababu majaji George Odunga na wenzake watano bado hawajaapishwa.

You can share this post!

Lowassa alazwa tena hospitalini baada ya kufanyiwa upasuaji

Isiolo Young Stars yapania kulea wengi kuchezea timu za...

T L