TUSIJE TUKASAHAU: Miradi ya unyunyiziaji maji imekwama

TUSIJE TUKASAHAU: Miradi ya unyunyiziaji maji imekwama

NA CHARLES WASONGA

MNAMO 2015 serikali ya Jubilee ilizindua miradi kadha ya kilimo cha unyunyiziaji katika maeneo kame ya North Rift katika mpango wa kuzipa jamii za wafugaji njia mbadala ya kuchuma mapato.

Mpango huo pia ulilenga kuimarisha uzalishaji chakula ili kudhibiti visa vya mashambulio ya kila mara yanayotekelezwa na wezi wa mifugo na wahalifu wengine.

Lakini serikali ya Rais Uhuru Kenyatta isije ikasahau kuwa miaka saba baadaye, miradi ya unyunyiziaji kama vile; ule wa Sigor Wei Wei ulioko Kaunti ya Pokot Magharibi na uliogharimu Sh1.2 bilioni, umekwama.

Mradi huo, ambao ulilenga kuweka ardhi ya ukubwa wa ekari 325, ulizinduliwa na Rais Kenyatta mwenyewe mnamo Septemba 7, 2015.

You can share this post!

Raila na Ruto wazidi kulisha Wakenya ahadi hewa

Ruto alilia ICC kuhusu hatari ya fujo kuzuka kwa kampeni

T L