TUSIJE TUKASAHAU: Mradi wa maji Nakuru haujakamilika kama ilivyoahidi serikali

TUSIJE TUKASAHAU: Mradi wa maji Nakuru haujakamilika kama ilivyoahidi serikali

NA CHARLES WASONGA 

MNAMO Machi 30, 2021 Waziri wa Maji Sicily Kariuki aliwahakikishia wakazi wa Nakuru na miji ya karibu kwamba ujenzi wa bwawa la Itare ungekamilika Novemba mwaka huo.

Hii, kulingana na waziri huyo, ni baada ya kurejelewa kwa shughuli za ujenzi katika mradi huo baada ya maelewano kati ya serikali za Kenya na Italia.

Waziri Kariuki asije akasahau kuwa, mradi huo unaogharimu Sh34 bilioni, ambao ulianzishwa mnamo 2014, bado haujakamilika alivyoahidi.

Wakazi wa mji wa Nakuru, ambao juzi ulipandishwa hadhi hadi kuwa jiji, na wale wanaoishi katika maeneo ya Njoro, Molo, Rongai, Elburgon, Bahati na Gilgil, bado wanakumbwa na kero la uhaba wa maji.

  • Tags

You can share this post!

Polisi wasaka wanaotupa miili Yala

Watu wachache wajitokeza kujiandikisha IEBC ikisaka kura...

T L