TUSIJE TUKASAHAU: Mudavadi ajue Ruto ni sehemu ya serikali anayoishambulia

TUSIJE TUKASAHAU: Mudavadi ajue Ruto ni sehemu ya serikali anayoishambulia

MNAMO Jumapili, kiongozi wa chama cha Amani National Congress (ANC), Bw Musalia Mudavadi, aliisuta serikali ya Rais Uhuru Kenyatta kuchangia ugumu wa maisha unaowakumba Wakenya wakati huu kwa kuendeleza ufisadi, ukopeshaji kupita mipaka na usimamizi mbaya wa uchumi.

Lakini asije akasahau kuwa rafiki yake mpya, Naibu Rais William Ruto, ni sehemu ya serikali ya sasa ambayo anadai inaendeleza maovu hayo ambayo anadai yamechangia taifa hili kuwa fukara.

Hii ni kwa sababu, kwa mujibu wa katiba ya sasa, Rais Kenyatta na Dkt Ruto, walichaguliwa kwa tiketi moja. Maovu ambaye Bw Mudavadi anadai, anarejelea yalitendeka wakati wa muhula wa kwanza wa utawala wa Jubilee, kabla ya Dkt Ruto ‘kutengwa serikalini’.

Kwa mfano, mnamo Novemba 2015, Dkt Ruto alitetea hatua ya serikali ya kuchukua mkopo wa Eurobond wa kima cha Sh256 bilioni akidai pesa hizo zilitumika kufadhili miradi ya ujenzi wa miundo msingi.

Hii ni licha ya malalamishi kutoka kwa viongozi wa upinzani, na Wakenya kwa ujumla, kwamba pesa hizo ziliporwa na maafisa wa serikali.

  • Tags

You can share this post!

CHARLES WASONGA: Sheria zilizoko zitumiwe kudhibiti sekta...

Vijana wazindua kampeni ya kutoa uhamasisho wa uandikishaji...

T L