TUSIJE TUKASAHAU: Rais afaa kutatua tatizo la wakulima wa miwa kabla ya kung’atuka madarakani

TUSIJE TUKASAHAU: Rais afaa kutatua tatizo la wakulima wa miwa kabla ya kung’atuka madarakani

NA CHARLES WASONGA

MNAMO Oktoba 3, 2015 Rais Uhuru Kenyatta aliahidi kuwa serikali yake itafanikisha mpango wa ubinafsishaji wa kampuni tano za kutengeneza sukari zilizoko magharibi mwa Kenya.

Hizo ni; Chemilil, Muhoroni, Sony, Nzoia na Miwani, ambazo zinamilikiwa na serikali.

Akiongea alipofungua rasmi Maonyesho ya Kilimo ya Kimataifa ya Nairobi, kiongozi wa taifa aliongeza kuwa serikali yake ingefutilia mbali deni la kima cha Sh39.7 bilioni zilizokuwa zikidaiwa kampuni hizo wakati huo.

Rais Kenyatta asije akasahau kuwa miaka saba baadaye, shughuli ya ubinafishaji wa kampuni hizo haijakamilika, na wakulima wanadai mamilioni ya fedha kutoka kwa kampuni hizo na kilimo cha miwa kimedumaa.

Huku ikisalia miezi sita kabla ya Rais Kenyatta kuondoka afisini wakulima wa miwa magharibi mwa Kenya wanaitaka serikali yake ikamilishe mpango huo unaolenga kuwafaidi.

  • Tags

You can share this post!

Viwanda vyafungwa mahindi yakikosekana

Polisi sasa kumfungulia shtaka mwanamume aliyeua watu 8

T L