TUSIJE TUKASAHAU: Rais atimize ahadi ya kuilinda mipaka yetu

TUSIJE TUKASAHAU: Rais atimize ahadi ya kuilinda mipaka yetu

HALI ya usalama katika sehemu kadha za Kaunti ya Lamu haijakuwa shwari kwa muda mrefu kutokana na mashambulio ya kigaidi ambayo yamesababisha maafa, uharibifu wa mali na wakazi kutoroka makwao.

Mojawapo ya sababu zinazochangia kuzorota kwa usalama katika kaunti hiyo, ilivyoshuhudiwa juzi, ni kwamba inapakana na taifa la Somalia ambalo ni ngome ya kundi la wapiganaji wa Al-Shabaab.

Kuzorota kwa uhusiano kidiplomasia kati ya Kenya na Somalia imeripotiwa kuwa mojawapo ya sababu zinazochangia utovu wa usalama Lamu, na maeneo mengi ya mpaka wa mataifa hayo mawili.

Lakini huku serikali ikiendeleza operesheni ya kupambana na wahalifu na magaidi Lamu, Rais Uhuru Kenyatta asije akasahau kuwa mnamo Oktoba 21, 2021 aliahidi kuwa Kenya itatatua mzozo wa mpaka katika bahari Hindi, “diplomasia”.

Hata hivyo, hajasema lolote kuhusu suala hilo tangu wakati huo kufikia sasa.

Rais Kenyatta alitoa ahadi hiyo alipokatalia mbali uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa kuhusu Haki (ICJ) ambayo katika uamuzi wake kuhusu mvutano huo, iliipa Somalia sehemu kubwa ya eneo linalozozaniwa.

  • Tags

You can share this post!

Viongozi wa Taita wazozana kuhusu ni nani bora machoni mwa...

Kalonzo alaani ubomoaji katika mtaa wa Mukuru

T L