TUSIJE TUKASAHAU: Ruto atueleze jinsi atakavyozima ufisadi Sh100 bilioni zikiwa kwa kapu la mikopo nafuu

TUSIJE TUKASAHAU: Ruto atueleze jinsi atakavyozima ufisadi Sh100 bilioni zikiwa kwa kapu la mikopo nafuu

NAIBU Rais William Ruto ameahidi kutenga Sh100 bilioni katika hazina maalum za kutoa mikopo nafuu kwa biashara ndogondogo za vijana na makundi mengine ya walalahoi, iwapo atachaguliwa kuwa rais hapo Agosti 9.

Lakini tusije tukasahau ni serikali hii, ambayo Dkt Ruto aliunda pamoja na Rais Uhuru Kenyatta 2013, iliyobuni Hazina ya Uwezo na kuitengea Sh6 bilioni ambazo zilinuiwa kutolewa kama mikopo ya kibiashara kwa vijana, akina mama na watu wanaoishi na ulemavu.

Vile vile, serikali ilibuni Hazina ya Ustawi wa Biashara za Wanawake (WEDF) na Hazina ya Ustawi wa Biashara za Vijana (YEDF) ambazo zilitengewa mabilioni ya fedha.

Hata hivyo, hazina hizo zimezongwa na ufisadi na kushindwa kufikia malengo yao.

Je, ni mikakati ipi Dkt Ruto ataweka kuzuia wafisadi kupora Sh100 bilioni atakazotenga kwa ajili ya kupiga jeki biashara za vijana?

  • Tags

You can share this post!

Ruto anamtaja naibu leo naye Raila ni kesho

Kocha McCrath kutegemea ujuzi wake kuvumisha Kenya Sevens

T L