TUSIJE TUKASAHAU: Ruto hajatimiza ahadi kuhusu bima ya NHIF

TUSIJE TUKASAHAU: Ruto hajatimiza ahadi kuhusu bima ya NHIF

AKIENDESHA kampeni maeneo mbalimbali ya nchi kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Agosti 9, Rais William Ruto aliahidi kuwa akishinda, Wakenya wote watasajiliwa katika Bima ya Kitaifa ya Matibabu (NHIF).

Alikariri, kila mara, kwamba serikali yake itatimiza ahadi hiyo kabla ya Desemba 1 mwaka huu, kama sehemu ya mpango wake wa kutimiza ajenda ya Afya kwa Wote (UHC).

“Kabla ya Desemba 2022, kila mmoja wenu atakuwa na bima ya NHIF. Wale ambao ni masikini watalipiwa na serikali na wale wenye uwezo wa kujilipia watashurutishwa kujilipia. Gharama yote ya matibabu italipiwa kupitia bima ya NHIF,” Dkt Ruto akasema mnamo Machi 22, alipokuwa akiendesha kampeni katika kaunti ya Nyamira.

Lakini Rais Ruto akiwa ametimiza ahadi ya kuanzisha hazina ya mahasla ya Hustler Fund, hajasema lolote kuhusu ahadi hii ya bima ya NHIF.

Hii ni licha ya Wakenya wengi, haswa maskini, kukabiliwa na changamoto kubwa katika jitihada zao za kugharamia matibabu

You can share this post!

Mume asimulia jinsi mke alivyomdunga mtoto wao kisu

Mbunge ataka wakongwe walindwe kwa njia bora

T L