TUSIJE TUKASAHAU: Sakaja atueleze jinsi anavyopanga kumaliza kero ya chokoraa jijini

TUSIJE TUKASAHAU: Sakaja atueleze jinsi anavyopanga kumaliza kero ya chokoraa jijini

KWA mujibu wa sensa kuhusu jamii za barabarani iliyofanywa mnamo Aprili 2018 na Wizara ya Leba na Masuala ya Kijamii, kuna jumla ya watu 15,337 wanaoishi barabarani.

Kulingana na ripoti hiyo, Nairobi ndio inaongoza na idadi ya watu hao, maarufu kama chokoraa, miongoni mwa kaunti zote 47, zenye idadi jumla ya watu 46, 629 kama hao.

Wizara hiyo ilisema idadi ya chokoraa inaongezeka kila uchao, haswa katika jiji la Nairobi ambako wao hufurika kusaka riziki.

Lakini watu hawa wamegeuka kuwa kero katika jiji hili kwani wao huwasumbua wakazi na kuwaibia mchana peupe, haswa katika barabara za Moi Avenue, Kimathi, Tom Mboya na Kirinyaga Road.

Akizuru sehemu kadha za Nairobi mnamo Agosti 27, siku mbili baada ya kuapishwa, Gavana Johnson Sakaja, aliahidi kuwa serikali yake itawaondoa chokoraa hao na kuwapeleka katika vituo vya kuwatunza.

Lakini mwezi mmoja baadaye, hajatoa taarifa yoyote kuhusu suala hilo ilhali wakazi wanaendelea kuhangaishwa na chokoraa kila leo.

  • Tags

You can share this post!

Gachagua apingwa kuhusu kauli ya misitu

WANDERI KAMAU: Hivi ndivyo tutakavyojiokoa kutoka katika...

T L