TUSIJE TUKASAHAU: Uvutaji wa sigara maeneo ya umma unahatarisha maisha ya wananchi

TUSIJE TUKASAHAU: Uvutaji wa sigara maeneo ya umma unahatarisha maisha ya wananchi

KUNA mwafaka miongoni mwa wataalamu wa afya kwamba uvutaji sigara unasababisha madhara mengi ya kiafya, kama vile, kansa ya mapafu.

Nchini Kenya, uraibu huu unasababisha zaidi ya asilimia 70 ya visa vya maradhi ya kansa ya mapafu, kulingana na Mwongozo wa Kitaifa kuhusu Udhibiti wa Kansa.

Lakini licha ya uwepo wa hatari hii, Wizara ya Afya inayoongozwa na Mutahi Kagwe na Wizara ya Usalama iliyoko chini ya Fred Matiang’i zimeonekana kuzembea katika wajibu wao wa kufanikisha utekelezaji wa Sheria ya Udhibiti wa Tumbaku ya 2007 inayopiga marufuku uvutaji sigara hadharani.

Uchunguzi wa safu hii umebaini kuwa waraibu wa sigara wamerejelea mwenendo wa zamani wa kuvuta sigara hadharani au maeneo ya umma, hali inayohatarisha maisha ya wananchi.

Mawaziri hawa wasije wakasahau kuwa wizara zao zina wajibu wa kufanikisha na kudumisha utekelezaji wa sheria hii ya udhibiti wa matumizi ya bidhaa za tumbaku.

  • Tags

You can share this post!

Ghasia zazuka Somaliland upinzani ukisisitiza kura ifanyike

TAHARIRI: Serikali ijayo isuluhishe upesi mzozo na FIFA,...

T L