TUSIJE TUKASAHAU: Wadau wahusishwe kikamilifu kuangazia changamoto ibuka za mfumo wa CBC

TUSIJE TUKASAHAU: Wadau wahusishwe kikamilifu kuangazia changamoto ibuka za mfumo wa CBC

MNAMO Mei 17, 2019, Waziri wa Elimu Prof George Magoha alitangaza kuwa Wizara ingeendelea kuandaa mikutano na wadau kujadili changamoto ibuka katika utekelezaji wa mtaala mpya wa masomo wa CBC.

Lakini mpaka sasa Prof Magoha hajatimiza ahadi hiyo.

Juzi Wizara pamoja na Tume ya Huduma za Walimu (TSC) zilitangaza kuwa walimu 650 watapewa mafunzo kwa ajili ya kufanikisha utekelezi wa CBC katika shule za upili.

Lakini vyama vya kutetea maslahi ya walimu, Knut na Kuppet, vinalalamika kutohusishwa katika maandalizi ya mafunzo hayo.

Waziri asije akasahau kwamba ni kinyume cha kipengele 118 cha Katiba kwa asasi yoyote ya serikali kutekeleza miradi au mpango wowote bila kuhirikisha wadau na umma kwa ujumla.

Kwa hivyo, na ili kutatua changamoto kadhaa zinazokumba utekelezaji wa mtaala huo mpya, sharti Waziri Magoha ashirikishe wadau wote.

Ujenzi wa madarasa mapya pekee hautoshi kufanikisha CBC, ambayo inatarajiwa kuingia katika shule za upili mwaka ujao.

  • Tags

You can share this post!

Wadau wataka serikali ifufue mpango wa chakula kwa wanafunzi

Uchafuzi wa mazingira huua watu 9m – Ripoti

T L