TUSIJE TUKASAHAU: Wafanyabiashara jijini Nairobi wanakumbusha NMS izindue masoko yaliyokamilika

TUSIJE TUKASAHAU: Wafanyabiashara jijini Nairobi wanakumbusha NMS izindue masoko yaliyokamilika

MNAMO Aprili 2021, Shirika la Huduma za Jiji la Nairobi lilianzisha mradi wa uboreshaji wa masoko manane ya wazi jijini Nairobi.

Mradi huo ulihusisha ujenzi wa vibanda vya kisasa vya kufanyia biashara, maeneo ya kuegesha magari, vyoo vya kisasa na barabara ndogo za kuelekea katika masoko hayo.

Miongoni mwa masoko yaliyolengwa kuboreshwa, chini ya mradi huo ni pamoja na Soko la Muthurwa, Soko la City Park, Soko la Jericho, Soko la Wakulima, Soko la Toi lililoko mtaa wa Kibera, miongoni mwa masoko mengine.

Mkurugenzi wa NMS Luteni Jenerali Mohamed Badi alitangaza kuwa mradi huo unalenga kupanua nafasi za biashara kwa wakazi wa Nairobi, ambazo, awali, zilikuwa finyu.

Hata hiyo baadhi ya wafanyabiasha wanamkumbusha Luteni Badi kuwa masoko matatu katika maeneo ya Mwariro, Westlands na Karandini ambayo yaligharimu Sh2.2 bilioni, yalikamilishwa Oktoba, 2021 lakini mpaka sasa hayajazinduliwa rasmi.

Wanaomba NMS izindue masoko haya kabla ya kipindi chake cha kuhudumu kukamilika Juni 9, 2022.

  • Tags

You can share this post!

SHINA LA UHAI: Hili eneo, ujauzito ni sawa na kitanzi!

Waliokosa kupata tiketi za Jubilee walia kuonewa

T L