TUSIJE TUKASAHAU: Wakulima wanaomba Nzoia Sugar iwalipe pesa kabla Uhuru astaafu

TUSIJE TUKASAHAU: Wakulima wanaomba Nzoia Sugar iwalipe pesa kabla Uhuru astaafu

MAELFU ya wakulima wa miwa katika Kaunti ya Bungoma wameitaka serikali kuu iwalipe pesa ambazo wanaidai kampuni ya sukari ya Nzoia.

Wiki jana, wakulima hao wakiongozwa na Jack Munialo, walisema kuwa wanaidai kampuni hiyo jumla ya Sh750 milioni, ambazo ni malimbikizo ya tangu mwaka wa 2019.

Wanadai kiasi hiki cha fedha baada ya serikali kutoa Sh500 milioni Januari 2021 kwa ajili ya kuwalipa.

Wakulima hao wanalalamika kuwa licha ya Rais Uhuru Kenyatta kuamuru mwaka 2021 kuwa Hazina ya Kitaifa itoe Sh1.5 bilioni za kutumika kulipa pesa ambazo wakulima wanadai kampuni za sukari za serikali, hawajapokea fedha hizo.

Rais Kenyatta alitoa tangazo hilo mnamo Oktoba 20, 2021 katika sherehe ya kitaifa ya Mashujaa Dei iliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Wang’uru, Kaunti ya Kirinyaga.

Sasa wakulima hawa wanamkumbusha Rais Uhuru Kenyatta kwamba amri yake haikutimizwa.

Wanaomba walipwe pesa hizo kabla ya kiongozi huyu wa taifa kuondoka afisini mwezi ujao wa Agosti.

You can share this post!

CAF yasukuma mbele fainali za AFCON 2023 kwa mwaka mmoja...

PAUKWA: Bahati machozi tele kwa aibu ya mamaye

T L