TUSIJE TUKASAHAU: Wavuvi walioathirika na ujenzi wa Lapsset walipwe fidia bila masharti yoyote

TUSIJE TUKASAHAU: Wavuvi walioathirika na ujenzi wa Lapsset walipwe fidia bila masharti yoyote

MNAMO Mei 1, 2018 Mahakama Kuu iliamuru serikali ilipe Sh1.76 bilioni kama fidia kwa wavuvi 4,600 katika kaunti ya Lamu walioathirika na ujenzi wa bandari mpya ya Lamu.

Wakitoa uamuzi huo katika mahakama ya Malindi, majaji; Pauline Nyamweya, Joel Ngugi, Beatrice Jaden na John Mativo waliagiza kwamba fidia hio ilipwe ndani ya mwaka mmoja kuanzia siku hiyo.

Walishikilia kuwa ni haki ya wavuvi hao kulipwa fidia hiyo kwa kupokonywa haki yao ya kuendesha shughuli zao katika eneo kulikojengwa bandari hiyo.

“Serikali itakuwa ikivunja haki za wavuvi hawa ikiwa itafeli kuwalipa fidia baada ya kutwaa sehemu ambayo wamekuwa wakiendesgha shughuli zao za uvuvi kwa miaka mingi,” majaji wakasema.

Lakini zaidi ya miaka mitatu baadaye serikali, kupitia Mamlaka ya Bandari Nchini (KPA), haijawalipa wavuvi hao pesa hizo, ambazo tayari zimetolewa na Hazina Kuu.

KPA ikumbuke kuwa ni wajibu wake kutoa pesa hizo kwa wavuvi hao bila masharti yoyote.

You can share this post!

Wadau wa utalii waonya wanasiasa dhidi ya kuzua vurugu...

Wambui aleta dhahabu ya 2 Olimpiki ya Viziwi 2022

T L