Tusker FC, Wazito na Police zazoa ushindi

Tusker FC, Wazito na Police zazoa ushindi

Na CECIL ODONGO

TUSKER jana ilianza safari ya kujifufua ligini huku Wazito na Kenya Police zikivuna ushindi mkubwa dhidi ya Mathare United na Bidco United mtawalia katika mechi zao za raundi ya 10.

AFC Leopards nayo inazidi kuandamwa na mawimbi ya kupata sare msimu huu, baada ya kupoteza uongozi wa 1-0 dhidi ya FC Talanta na kulazimishiwa sare ya 1-1 ugani Nyayo.

Tusker ilipata ushindi wake wa tatu kwa kuilemea Nzoia Sugar 1-0 katika uga wa Sudi, Kaunti ya Bungoma. Mshambuliaji raia wa Uganda Deogratious Ojok alifunga bao hilo pekee dakika ya 29 na kuzima kabisa matumaini ya Nzoia ambayo wiki jana iliipiga Kariobangi Sharks 3-0 na kusajili ushindi wake wa kwanza msimu huu.

Kennedy Ochieng’ alifungia Mathare United bao la kufutia machozi.? Ugani Utalii, Wazito ilivuna ushindi mkubwa zaidi wikendi kwa kuilemea Mathare United 4-1. Beki Musa Masika alitinga mabao mawili huku Elly Asieche na Vincent Oburu pia wakipata bao moja kila moja.

Wimbi hilo la ushindi liliendelea hata katika uga wa Kasarani Annex ambako Kenya Police iliadhibu Bidco United 3-0. Cliftone Miheso alifunga kupitia mkwaju wa penalti baada ya Kassim Mwinyi kunawa mpira katika eneo la hatari wakati alipokuwa akizuia krosi ambayo pia ilimegwa na Miheso.

Clinton Kinanga aliongeza la pili dakika ya 42, akiachilia shuti kali ndani ya kijisanduku kabla ya Charles Ouma kuongeza la tatu dakika ya 56.Ugani Nyayo, Ingwe ilipoteza alama kwa mara nyingine, ilipotoka sare ya 1-1 dhidi ya FC Talanta.

Daniel Musamali aliipa Ingwe uongozi kunako dakika ya 10 kipindi cha kwanza kabla ya Edwin Lavatsa kusawazishia Ingwe kipindi cha pili.Kutokana na ushindi dhidi ya Nzoia, Tusker ilipaa hadi nafasi ya 12 kwa alama 10 baada ya kujibwaga uwanjani mara saba.

Nzoia ambayo ilipata ushindi wake wa kwanza kwa kuilemea Kariobangi Sharks 3-0 wikendi ya juzi nayo sasa imeporomoka hadi 17 kwa alama sita baada ya mechi tisa.Kenya Police nayo iliruka hadi nafasi ya 11 kwa alama 11 baada ya mechi 10 huku Bidco United ikiporomoka hadi 13 kwa alama 10 baada ya 10.

Ingwe nayo bado inaselelea katika nafasi isiyoridhisha ya 15 kwa alama tisa huku FC Talanta ikiwa nambari saba kwa alama 16, timu zote zikiwa zimecheza mechi 10.Wazito imepaa hadi nafasi 14 kwa alama tisa, Mathare United ikiporomoka hadi nafasi ya 16 kwa saba ikiwa timu hizo mbili zimejibwaga uwanjani mara 10.

You can share this post!

Wadadia wagaragaza Bunyore ligi kuu KWPL ikianza kwa...

Kenya yapigiwa debe kuandaa Riadha za 2025

T L