Michezo

Tusker yamtema Osumba

November 15th, 2018 1 min read

NA CECIL ODONGO

MABINGWA mara 11 wa KPL Tusker FC wamemwachilia mchezaji wao nyota, kiungo mkabaji Brian Osumba ambaye alikuwa mhimili mkubwa kikosi mwao msimu uliopita wa 2017/18.

Osumba aliwasaidia Wanamvinyo hao  kumaliza katika nafasi ya tatu ligini na kuachiliwa kwake haukutarajiwa na mashabiki wengi wa timu hiyo.

Hata hivyo, mkufunzi wa Tusker FC  Robert Matano ametetea uamuzi wake  akisema mwanasoka huyo hayupo kwenye mipango yake ya baadaye na timu hiyo  na hawezi kufurahia akimkalisha benchi.

“Tuliamua kumwaachilia kwasababu hayupo kwenye mpango wetu wa msimu ujao. Vile vile si vyema kumweka benchi mchezaji anayejivunia ukwasi wa talanta kama yeye anayeweze kutamba kwingineko,” akasema Matano.

Taarifa hata hivyo zimedhibitisha kwamba Osumba atajiunga na wanabenki KCB huku nafasi yake ikitwaliwa na Clyde Seneji aliyewaga wino kwenye  kataba wa muda wa miaka mitatu na Wanamvinyo hao akitokea Thika United iliyoshushwa daraja mwishoni mwa msimu  wa 2017/18.

Vile vile kocha huyo amefichua kwamba tTusker FC imekamilisha usajili wa wachezaji wapya na watashawishika kuendelea tu iwapo watapata mwanasoka mzuri ajabu anayejivunia talanta ambayo hawana.