Twaha Mbarak akutana na Origi Anfield baada ya Liverpool kushinda Wolves

Twaha Mbarak akutana na Origi Anfield baada ya Liverpool kushinda Wolves

NA JOHN ASHIHUNDU

TWAHA Mbarak anayewania kiti cha urais kwenye uchaguzi ujao wa FKF ni miongoni mwa Wakenya waliopata fursa ya kuhudhuria mechi kati ya Liverpool na Wolves ambapo alipata fursa ya kuzungumza na Divock Origi mara tu pambano hilo lilipomalizika.

Origi ameagana rasmi na Liverpool na kuhamia AC Milan ya Italia.

Mbelgiji huyo mwenye umri wa miaka 27 alizaliwa Ostend nchini Ubelgiji na kulelewa Houthalen-Oost.

Lakini hakucheza Jumapili kutokana na jeraha la muda mrefu.

Mbarak alihudhuria sherehe za kumuaga rasmi Origi ugani Anfield baada ya kualikwa na staa huyo ambaye babake Mike Okoth alicheza soka ya kulipwa nchini Ubelgiji, mbali na kuwa nahodha wa Harambee Stars miaka ya hapo awali.

“Origi amejawa na furaha tele baada ya kupata fursa ya kucheza soka ya Serie A, na sasa anajiandaa kufanyiwa vipimo vya kimatibabu kabla ya kusajiliwa rasmi. Kocha Jurgen Kloop ni shabiki mkubwa wa Origi, lakini hakuwa akimpa fursa ya kutosha kikosini.”

Kadhalika Mbarak alisema Origi ameamua kuondoka ili ajiunge na timu ambayo itampa nafasi ya kutosha ili apate nafasi katika kikosi cha timu ya taifa cha Ubegiji kinachojiandaa kwa fainali za Kombe la Dunia za 2022.

Twaha Mbarak (kati) anayewania kiti cha urais kwenye uchaguzi ujao wa FKF akiwa na Divock Origi na mamake Origi, Bi Linda, baada ya mechi ya Liverpool dhidi ya Wolves. PICHA | HISANI

Baada ya kutwaa ubingwa wa Serie A, AC Milan imemhakikishia Origi nafasi katika kikosi kitakachoshiriki mechi za Klabu Bingwa barani Ulaya msimu ujao.

Origi ameahidi kuzuru Kenya hivi karibuni na kuzungmza na washikaji dau wa kandanda kwa jumla.

“Tulizungmza mambo mengi kuhusu uongozi wa kandanda nchini, na jinsi tunavyoweza kuubadilisha kwa manufaa ya taifa lote,” alisema Mbarak.

Origi alifunga mabao matatu katika mechi saba dhidi ya West Ham United, Wolves na Everton.

  • Tags

You can share this post!

Man-City wakomoa Aston Villa ugani Etihad na kuhifadhi taji...

FAO yafanya majaribio ya mpango wa kudhibiti shughuli za...

T L