Habari Mseto

Ubalozi wa Angola nchini Kenya wafungua tovuti mpya

November 13th, 2019 1 min read

Na MAGDALENE WANJA

KATIKA juhudi ya kudumisha uhusiano mwema kati ya mataifa mawili, ubalozi wa Angola nchini Kenya umefungua tovuti ya kutoa habari.

Tovuti hiyo iliyofunguliwa Novemba 11, 2019, ilianzishwa pia kusheherekea siku ya uhuru (Independence Day) wa Angola.

Tovuti hiyo www.embassyofangolainkenya.org pia inaonyesha saa katika miji mikuu ya nchi hizo mbili, Nairobi na Luanda.

“Tovuti hiyo ni jukwaa la mawasiliano kati ya ofisi ya ubalozi na wananchi pamoja na kutoa habari muhimu kutoka ofisini humo,” ilisoma taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kwa ubalozi huo.

Kwa kutembelea tovuti hiyo, unaweza kupata habari mbalimbali kuhusu nchi ya Angola.

Hizi ni pamoja na habari za kila siku, jinsi ya kufanya biashara nchini Angola na wananchi wa Angola wanaoishi nchini Kenya.

“Tovuti hiyo pia ni njia ya rahisi ya kuwawezesha Wakenya kupata huduma za kidiplomasia kutoka nchini Angola,” ilisoma taarifa hiyo.

Kuzinduliwa huku kulifanyika pamoja na kuanzishwa kwa teknolojia mpya ambayo itasaidia katika utoaji wa huduma za visa.