Habari Mseto

Uber Chap Chap yajivunia kuimarika kwa biashara

November 1st, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Idadi ya magari ya Uber Chap Chap imeongezeka kwa asilimia 150 tangu yalipoanza kuhudumu Februari.

Kufikia sasa, magari hayo ni 500 kutoka 200 miezi nane iliyopita.

Ripoti hii ni kwa mujibu wa Uber Jumatano.

Magari ya Uber Chap Chap, Suzuki Altos, hununuliwa kwa mkopo kutoka Stanbic Bank na hutumia mafuta vizuri.

“Mahitaji ya Uber ChapChap yamo juu sana. Madereva hufanya ziara nyingi zaidi kwa siku,” alisema meneja wa eneo la Mashariki ya Kati na Afrika Anthony le Roux.

Jumatano, Uber ilitia sahihi mkataba na watengenezaji magari, Suzuki, ili kuongoza hatua ya kuimarisha Uber ChapChap Nairobi na kuanzisha programu kama hiyo katika mataifa mengine Barani Afrika.

Uber inalenga madereva 6,000 ambapo madereva wengi hutumia magari ya kukodisha.