Habari Mseto

Uber kuwatuza madereva wake

April 18th, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Kampuni ya teksi Uber kwa kushirikiana na kampuni zingine 10 imezindua tuzo kwa madereva wanaotoa huduma maalum.

Kampuni hiyo, inayopitia changamoto kuu hasa kutokana na ushindani mkali ilizindua ‘Uber Rewards’ kuwazawadi madereva wanaotumia apu yake.

Tuzo hiyo pia inawawezesha madereva kuwapunguzia wateja wao nauli lakini inawazawidi kuambatana na wakati wanaotumia kuendesha biashara kwa kutumia apu yao.

Kulingana na meneja wa Uber Greenlight hub, Kenya, Emmah Mutunga, kampuni hiyo ya kiteknolojia imejitolea kuwasaidia madereva wake katika kutimiza lengo la kampuni hiyo la kibiashara.

Kampuni na mashirika yanayoshirikiana na Uber GLH ni Mamlaka ya Uchukuzi na Usalama nchini, Mp Shah, Flare, Toyotsu, Huawei, Essilor, Kingsway, na Telkom Kenya.