Uchungu wa mama

Uchungu wa mama

Na SINDA MATIKO

ZILE tetesi kwamba Diamond Platnumz anatoka na Zuchu zimeonekana kumchefua mamake mrembo huyo, mkongwe wa Taarab Khadija Kopa.

Kwa muda sasa Diamond na Zuchu wamehusishwa kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi chini ya maji.

Zuchu alishapiga taarifa hizo kwa kusisitiza kuwa Diamond sio tu bosi wake lakini pia ni kama babake hivyo hawezi kutoka naye kimapenzi.

Lakini lile tukio la mwezi Desemba 2021 ambapo Diamond aliamua kumpeleka deti usiku, liliibua tena tetesi hizo na mpaka sasa zimegoma kupoa.

Taarifa hizi zimemfikia Khadija ambaye ndiye alimpeleka Zuchu kwa Diamond na kumwomba amsaini katika lebo yake ya Wasafi.

Khadija Kopa (kulia) ni malkia wa mipasho, mfanyabiashara mashuhuri, mwigizaji shupavu na mwimbaji maarufu wa muziki wa Taarab kutoka Tanzania. PICHA | CHRIS ADUNGO

Mwenyewe naye kabaki kushangaa huku akizikana.

“Diamond ameishi kuniita mama hata kabla ya binti yangu ajiunge na Wasafi. Uvumi huu umenishangaza sana na nilipousikia nilimuuliza binti yangu kama ni kweli. Alinithibitishia kuwa hana mpenzi kabisa. Uelewa wangu ni kuwa binti yangu na Diamond ni mandungu tu hivyo mazoea yao ni ya kindugu,” kafunguka.

Hata hivyo, anasema hana ishu akimpata mwanamume wa kumpenda sababu ni binti mkubwa ilimuradi tu jamaa awe mungwana.

  • Tags

You can share this post!

Kipchoge apigwa jeki na INEOS kutimka kwenye marathon...

Uhuru kuwa kocha mkuu wa ‘Team Raila’

T L