Uchunguzi duni huvuruga kesi zinazohusu polisi – Haji

Uchunguzi duni huvuruga kesi zinazohusu polisi – Haji

NA ERIC MATARA

MKURUGENZI wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji amesema kuwa kuvurugwa kwa uchunguzi, ushahidi pamoja na vitisho ni kati ya masuala ambayo yamevuruga upatikanaji wa haki hasa katika kesi ambazo zinahusisha dhuluma zilizotekelezwa na maafisa wa polisi.

Bw Haji alisema kupata haki kwenye kesi kama hizo ambapo maafisa wa usalama wamehusika kumekuwa vigumu kwa sababu ushahidi huwa umevurugwa.

Akizungumza wakati wa Kongamano la Kitaifa kuhusu Mageuzi na Uhalifu, Bw Haji alisema kuwa matumizi ya nguvu kupita kiasi, kukamatwa kwa watu kiholela na kuzuiliwa kwao bila makosa yoyote kumesababisha umma ukose imani katika utendakazi wa idara ya polisi hasa katika kuchunguza kesi mbalimbali.

Kongamano hilo liliandaliwa mjini Naivasha na liliwashirikisha washikadau mbalimbali.

“Hapo awali tumeshuhudia kuvurugwa kwa haki za raia kutokana na tabia ya polisi kutumia nguvu kupita kiasi. Kwa mfano kamatakamata za kiholela, uharibifu wa mali na kukosa kutambua kuwa mtu hana kosa hadi mkondo wa kisheria utamatike na pia kuwazuia watu kuwakilishwa kwenye kesi, ni kati ya matatizo makubwa ambayo huchangia ukosefu wa haki,” akasema Bw Haji.

Jaji Mkuu Martha Koome ambaye alikuwa mgeni wa heshima kwenye kongamano hilo, alisema idara ya mahakama inamakinika kutekeleza mageuzi mbalimbali ambayo yatahakikisha kuwa kuna haki.

  • Tags

You can share this post!

Salah na De Bruyne kati ya masogora wanane wanaowania taji...

Masuala nyeti ya Wakenya katika uchaguzi

T L