Habari Mseto

Uchunguzi kuhusu kifo cha msichana waanza

October 6th, 2020 1 min read

NA FAUSTINE NGILA

Mafisa wa DCI wameanzisha uchunguzi kubaini ni nini kilochosababisha kifo cha msichana wa miaka sita ambaye wazazi wake wawili walikuwa na mzozo.

Hii ni baada ya Habari kuibuka kwamba hakufariki kutokana na ugojwa wa dharura kama ilivyoripotiwa na babayake mwezi moja Zaidi ya mwezi moja uliopita.

Wazazi wa Berverly Mumo, Robison Musyoki na Naomi Kiamba wamekuwa kwa miaka tatu wakitembelea korti kila mmoja akiomba kupewa ruhusa ya kuishi na mtoto wao ambaye alikuwa miaka tatu wakati walitengana 2017.

Beverly alikuwa anaishi na baba yake Mlolongo kaunti ya Machakos wakati alifariki Agosti 24.

Kwenye ripoti iliyoandikishwa kwenye kituo cha  polisi cha Mlolongo msichana huyo alisema kwamba alikuwa anaumwa na kifua wakati alisemekana kufariki kwenye hospitali ya Mater Nairobi

Uchunguzi uliofanywa na madaktari  ulionyesha kwamba alifariki kwa maumivu.