Habari Mseto

Uchunguzi waanza baada ya polisi kupata mwili wa mwenzao chumbani kwake

October 31st, 2020 1 min read

NA FAUSTINE NGILA

Maafisa wa polisi kutoka mji wa Nyahururu wanachunguza kifo cha afisa mwenzao ambaye mwili wake ulipatakina chumbani kwake Kaunti ya Laikipia.

Konstabo wa polisi David Murai aliyekuwa akihudumu kwenye kituo cha polisi cha Nyahururu kwenye idara ya barabara alipatikana akiwa amefariki mtaa wa Garden Estate Ijumaa asubuhi.

Kulingana na kamanda wa polisi wa Nyahururu Geoffrey Mayek mwili wa afisa huyo alipatikana kwa kitanda ukiwa umefungwa Kamba shingoni.

Mkuu huyo wa polisi alisema kwamba maafisa upellezi wa zuilia mke wa Mwenda zake Selina Wambui amabye aliripoti kisa hicho huku akidai kwamba mmewe alijitia kitanzi nyumbani kwao.

 Mke wa mwendazake alikuwa nyumbani wakati tukio hilo lilitokea usiku huo kwani alipigia maafisa wa kituo hicho kuwa julisha kwamba mmewe alikuwa amejitia kitanzi.

“Alikamatwa kuhusiana na tukio hilo kwani haneweza kupena ripoti kamili ya kile kilichotokea,alisema mkuu huyo wa polisi.

Kulingana na ripoti za majirani afisa huyo na mkewe Wangui walikuwa na matatizo ya Ndoa .

“Wawili hao walikuwa na Watoto wawili huku mwa kitinda mimba akiwa na mwezi mmja wamekuwa wakizozana mara kwa mara,”Jirani aliambia Taifa Leo.

Mwili wake ulipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhi miti cha hospitali ya Nyahururu ukigoja upasuaji.