UDA yaondoa mamlakani maafisa walioteuliwa majuzi

UDA yaondoa mamlakani maafisa walioteuliwa majuzi

Na KIPKOECH CHEPKWONY

CHAMA cha United Democratic Alliance (UDA) chake Naibu wa Rais Dkt William Ruto kimetimua maafisa wake watano, mwezi mmoja baada ya kuwateua.

Kupitia taarifa iliyochapishwa katika Gazeti Rasmi la Serikali na Msajili wa Vyama vya Kisiasa Ann Nderitu, UDA kimefurusha Anthony Otieno Ombok aliyekuwa katibu wa mipango na nafasi yake ikachukuliwa na Karisa Nzai Munyika.

Mweka hazina wa kitaifa sasa atakuwa mbunge wa zamani wa Mugirango Kusini, Omingo Magara ambaye amechukua nafasi ya Bi Eddah Jebet Ruto.

Jamhuri Guyo Warda atachukua nafasi yake Mohammed Ishmael kama naibu katibu na mratibu wa shughuli za kitaifa.

Wakili Edward Muriu sasa atachukua nafasi yake Melisa Ngania kama katibu wa masuala ya sheria na nafasi yake Susan Nyawira aliyekuwa naibu mweka hazina itachukiliwa na aliyeliwa mwaniaji wa kiti cha useneta Kaunti ya Embu, Kanake Joshua Mugo.

You can share this post!

DIMBA: Harusi tunayo! Ya Trapp na Izabel

Mke kizimbani kwa madai alimmwagia ‘mpango’ petroli

T L