Makala

UDAKU: Jimenez aanzana na mwigizaji Basso

January 6th, 2020 1 min read

Na GEOFFREY ANENE

NI nadra sana kwa wanasoka maarufu kutoka kimapenzi na vichuna mashuhuri katika ulingo wa drama.

Ingawa hivyo, mambo ni tofauti kabisa kwa mwanasoka nyota mzawa wa Mexico, Raul Alonso Jimenez Rodriguez ambaye kwa sasa amepata hifadhi ya penzi lake moyoni mwa mwigizaji matata mzawa wa Amerika, Daniela Basso, 30.

Jimenez ambaye pia amewahi kuvalia jezi za Atletico Madrid ya Uhispania kati ya 2014 na 2015, kwa sasa huwasakatia Wolverhampton (Wolves) ya Uingereza kwa mkopo wa mwaka mmoja kutoka Benfica inayoshiriki Ligi Kuu ya Ureno.

Daniela ambaye awali alikuwa fundi hodari wa masuala ya ukahaba, kwa sasa ni mwigizaji wa haiba kubwa wa telenovela za mahaba almaarufu ‘Soap Operas’.

Hatua ya Jimenez kuanza kumtambalia Daniela kimapenzi inajiri miezi michache baada ya mwanasoka huyo kutemana na gwiji mkongwe wa masuala ya huba, Michele Anne Mason almaarufu Kendra Lust ambaye pia amewahi kumfungulia duka mwanasoka maarufu wa Real Madrid na timu ya taifa ya Colombia, James Rodriguez.

Mapema wiki jana, Jimenez mwenye umri wa miaka 28, alikiri kuvutiwa na ubora wa maumbile ya maziwa kifuani pa Daniela kuanzia 2018.

Ingawa hivyo, ilikuwa hadi mwezi jana ambapo alianza kuwa mwepesi wa kupakia mitandaoni picha alizopigwa kwa pamoja na kipusa huyo ambaye katika mahojiano yake na gazeti la ‘The Sun’, alikiri kufurahia jinsi anavyokunwa kila mara Jimenez anapolitalii buyu lake la asali.

Shabiki mmoja hata hivyo alimuuliza Jimenez jinsi humridhisha Daniela chumbani hasa ikizingatiwa historia ya kidosho huyo katika masuala ya ukahaba.