Habari Mseto

UDAKU: Kibarafu wa Eric Omondi adai yeye ndiye Baby Mama pekee

January 15th, 2024 1 min read

NA FRIDAH OKACHI

MPENZI wa msanii Eric Omondi, Lynne Njiha anasema kwamba yeye pekee ndiye aliyezalia mchekeshaji huyo.

Hivyo basi, Lynne anajigamba akidai yeye ndiye Baby Mama wa Eric Omondi.

Kwenye video aliyopakia Instagram wakati wa kujibu maswali ya mashabiki, mama huyo wa mtoto mmoja alisisitiza kuwa mchekeshaji huyo hana mtoto mwingine nje ya mahusiano yao.

Anaamini kuwa yeye pekee ndiye amefanikiwa kupata mtoto na msanii huyo.

“Hili swali ni ngumu lakini wacha ni jibu; Hapana, sijui. Hata hajui, hajui. Mimi pekee yangu ndiye niko (akimaanisha Baby Mama),” alisema Lynne huku akitabasamu.

Kwenye jukwaa hilo la maswali Instagram, aliulizwa iwapo kuna uwezekano wa kupanua familia yao.

Lynn alifichua kwamba kwa sasa hana haraka wa kupata mtoto mwingine.

“Kwa sasa, mimi ni mama wa mtoto mmoja aliye na baba mmoja!” Aliongeza.

Alifunguka akielezea mahusiano yake ambayo yana pengo kubwa ya kiumri na mchekeshaji huyo.

Lynne ana umri wa miaka 22, naye Eric Omondi 42.

“Nilikutana naye nikiwa na umri wa miaka 19, mwaka wa 2022. Naamini mapenzi ni mapenzi. Mapenzi hayana mipaka …Na iwapo unapenda mtu, kuwa na mahusiano naye,” alijibu Lynne.

“Mamangu hakuwa anatarajia kuwa niwe na mpenzi aliyenishida umri. Lakini amekuwa wa msaada mkuu kwangu. Kwa sababu huyo ndiye yuko,” alikamilisha Lynne.

Mwanadada huyo aliweka wazi kuhusu uhusiano wake kimapenzi na Eric Omondi Septemba 2022.

Mwaka huohuo, wawili hao walipoteza mtoto ambaye hakuwa amezaliwa.