Dimba

Udaku: Kisura atembea tupu tupu kuwapa ‘motisha’ Samba Boys

June 15th, 2024 2 min read

NA CHRIS ADUNGO

KIPUSA Tyffany Santos, ambaye huuza picha na video za uchi kwenye jukaa la OnlyFans, ameahidi kuwapa wanasoka na mashabiki wa timu ya taifa ya Brazil “burudani ya kipekee” iwapo kikosi hicho kitafaulu kutwaa taji la Copa America mwaka huu.

Tyffany aliahidi kwamba atavua nguo asalie uchi wa mnyama ili kusherehekea ufanisi wa Brazil, kwenye fainali itakayondaliwa ugani Hard Rock jijini Miami, Amerika, hapo Julai 14.

“Nitajitosa uwanjani tuputupu baada ya fainali hiyo ili mashabiki na wachezaji wapate burudani tosha,” alitanguliza kipusa huyo kwenye mtandao.

“Mambo yatakuwa tofauti na murua zaidi kwa Neymar na Vinicius Jr, ambao nitawaonjesha asali iwapo watatusaidia kubeba taji,” akaongeza.

Kisura huyo pia ameahidi kutia mchoro wa kudumu wa jina ‘NeyVini’ — ufupisho wa Neymar na Vinicius — kwenye makalio.

Vile vile, atachanja chale za sura za wanasoka hao wawili kifuani ili kuashiria penzi lake kwa masupastaa hao tegemeo kambini mwa Brazil.

Katika jaribio la kuwatia wawili hao kishawishini wiki hii, Tyffany alirekodi video akiwa uchi katika uwanja wa Underground jijini London.

Cha pekee kilichomsitiri ni rangi za bendera ya Brazil alizokuwa amepakwa mwilini.

Mtunzi na mtayarishaji huyo wa maudhui ya watu wazima alirekodi pia safari yake hiyo akiwa kwenye kituo cha treni cha Queensway, kabla kushukia kwenye kituo cha chini ya ardhi cha Piccadilly Circus ambapo alishangaza wengi wakiwemo watalii kutoka Brazil alipojifunika mwili kwa rangi zilizojichora kwa mtindo wa sare ya timu.

Alitumia muda wa zaidi ya saa nne kuchora mwili wake hadi akapata mwonekano huo, kituo cha Odia nchini Brazil kimefichua.

Juu alipakwa rangi za manjano na kijani kisha rangi ya bluu au samawati kwenye sehemu za chini ya mwili wake. Baadaye alisafiri kuzunguka jiji la London mbele ya watazamaji wengi.

Alirekodi pia safari yake hiyo akiwa kwenye kituo cha treni cha Queensway kabla ya kushukia kwenye kituo cha chini ya ardhi cha Piccadilly Circus, ambapo alishangaza wengi, wakiwemo watalii kutoka Brazil.

Akihojiwa, alisema hakulenga kuzua tafrani yoyote, bali alitaka kutoa heshima kwa timu ya taifa ya Brazil na kuonyesha mapenzi yake kwa Neymar na Vinicius Jr.

Alisema: “Nilitaka kutoa heshima kwa Brazil na kuonyesha najivunia usuli wangu kwa kuwa soka yetu haina kifani duniani kote. Mimi ni shabiki sugu mwenye shauku, si shabiki wa kawaida!”

Tyffany si mwanamitindo wa kwanza wa OnlyFans kuwahi kujipata kwenye hali kama hiyo.

Shabiki sugu wa Arsenal, Arabella Mia, naye aliwahi kujitoma ugani Emirates akiwa uchi wa mnyama mnamo Juni na Oktoba 2023 huku cha pekee kilichomsitiri ikiwa ni rangi za jezi za kikosi hicho cha Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).