Michezo

UDAKU: Mama mzazi wa Neymar Jr amtema mpenzi wake mwenye umri wa miaka 22

April 25th, 2020 1 min read

Na GEOFFREY ANENE

MAMA mzazi wa supastaa wa Paris Saint-Germain Neymar, Nadine Goncalves amekatiza uhusiano wa kimapenzi na mpenzi wake mpya mwenye umri wa miaka 23 siku 10 tu baada ya kuuanzisha.

Ripoti zinasema kuwa Nadine, ambaye ni rais wa taasisi ya michezo ya Neymar nchini Brazil na anafuatwa na watu 1.6 milioni kwenye mtandao wake wa Instagram, alichukua hatua ya kutema mwanamitindo huyo kwa jina Tiago Ramos baada ya kupata habari alikuwa shoga.

Majuzi, Nadine,52, ambaye alitalikiana na babaye Neymar mwaka 2016 baada ya kuwa kwenye ndoa miaka 25, aligonga vichwa vya habari alithibitisha uhusiano wao kwa kuchapisha picha yake na Ramos anayezidiwa kwa umri na mchezaji Neymar kwa miaka sita, wakiwa wameshikana na kuangaliana kimapenzi nje ya nyumba yake.

Hata hivyo, Nadine sasa ameamua kumpiga teke Ramos baada ya kugundua alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume kadhaa wakiwemo mpishi mkuu wa Paris Saint-Germain Mauro pamoja na muigizaji Mbrazil Carlinhos Maia kabla ya kukutana naye.

Tiago, ambaye ana wafuasi 652, 000 kwenye Instagram, aliwahi kupigwa picha katika karamu ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Neymar mwezi Februari.

Walipotangaza uhusiano wao, Neymar alitakia mamaye furaha katika hatua aliyokuwa amechukua. Hajazungumzia habari za hivi punde za mamaye kutema Tiago.