Michezo

UDAKU: Ni wazi Neymar anakula bata na Paola

December 30th, 2019 1 min read

Na MWANDISHI WETU

NYOTA Neymar Jr amefichua kwamba anatoka kimapenzi na mwigizaji maarufu mzawa wa Mexico, Danna Paola, 24.

Hii ni baada ya mvamizi huyo wa PSG na timu ya taifa ya Brazil kukiri kwamba kichuna huyo anazitesa hisia zake kutokana na urembo aliojaliwa.

Mwazoni mwa wiki jana, Neymar alionekana pamoja na Paola wakipigwa picha za pamoja zilizopakiwa na kidosho huyo mitandaoni.

Kwenye mojawapo ya picha, videge hao walionekana wakiponda raha katika mkahawa mmoja jijini Paris, Ufaransa. Mbali na kupigana mabusu, Neymar alikuwa akiyapapasa maziwa ya gwiji huyo wa filamu huku naye akijilegeza kwa dume lake.

Chini ya picha hizo, Paola aliandika “Heri njema za Krismasi mpenzi”, naye Neymar akajibu “Asante sana malkia”, jumbe ambazo ziliibua gumzo kubwa miongoni mwa mashabiki wa wawili hao kwenye mtandao wa Instagram. Danna anaanza kumfungulia Neymar buyu lake la asali baada ya mwanasoka huyo kutemana na aliyekuwa mpenzi wake wa miaka sita, Bruna Marquezine.

Awali, fowadi huyo wa zamani wa Barcelona alikuwa akiitalii mzinga wa mwanamitindo Mari Tavares kabla ya kukiri kuvutiwa na maungo ya Ellen Santana aliyetawazwa mshindi wa Miss BumBum nchini Brazil mnamo 2018.

Ni miezi miwili tu imepita tangu Neymar atemane pia na mwanamitindo Noa Saez aliyekuwa mwenyeji wake wa mara kwa mara katika mkahawa wa Mr Porter jijini Catalonia, Uhispania.

Noa aliingia katika orodha ndefu ya vichuna wa Neymar baada ya sogora huyo kuburudishwa pia na warembo Mari Tavares wa Brazil, Liza Brito kutoka Uswisi na Larissa ‘Anitta’ Macedo wa Brazil.