BambikaMakala

Udaku: Nitakuwa tajiri tajika duniani, Diamond asema

Na WINNIE ONYANDO September 5th, 2024 1 min read

MWANAMUZIKI mashuhururi duniani Diamond Platnumz amefichua kuwa ndoto yake ni kuwa tajiri tajika ulimwenguni.

Akizungumza Jumanne, Septemba 3, 2024 wakati wa uzinduzi wa Wasafi Festival Makala 2024, mwanamuziki huyo alisema kuwa hivi karibuni atazindua baadhi ya projekti zake zitakazompandisha hadhi na kuinua mapato yake.

“Ndoto yangu kubwa maishani ni kuwa mtu tajiri zaidi duniani. Hiyo ni ndoto yangu na ninaweza kukuhakikishia kuwa nitakuwa tajiri mkubwa zaidi duniani,” Diamond alisema.

Diamond aliwaeleza wafuasi wake kuwa hapo nyuma alitaka kumiliki gari aina ya Rolls Royce na haikuchukua muda na akalinunua, hivyo hakuna kitakachomzuia kuwa tajiri tajika duniani.

 “Na niwahakikishia kuwa nitakuwa Mtanzania ambaye ataiwakilisha nchi yake kuwa tajiri mkubwa duniani,” alisema.

Kando na hayo, alisema kuwa baadhi ya projekti atakazozindua zitapendwa na wengi.

“Mwaka huu, 2024, natambulisha bidhaa mpya ambayo itakuwa miongoni mwa wadhamini wa Wasafi Festival na pia niwahakikishie itakuwa ni bidhaa inayopendwa na watu wengi na watakuwa na hamu ya kuipata na nataka mniunge mkono wakati huo,” akaongeza.

Kwa sasa, Diamond ni miongoni mwa wanamuziki matajiri zaidi barani Afrika.

Anamiliki WCB Wasafi.

Pia, anamiliki Tamasha la kila mwaka liitwalo Wasafi Festival ambalo hufanyika Tanzania.