Uefa yakunja mkia kuadhibu Barcelona, Real Madrid na Juventus kuhusu kipute kipya cha European Super League

Uefa yakunja mkia kuadhibu Barcelona, Real Madrid na Juventus kuhusu kipute kipya cha European Super League

Na MASHIRIKA

VIKOSI 12 vilivyojaribu kuagana na Shirikisho la Soka la Bara Ulaya (Uefa) kwa azma ya kuunda kipute kipya cha European Super League (ESL) sasa vimesamehewa.

Ingawa hivyo, Uefa imeahidi kukabiliana na klabu hizo kisheria kwa njia nyingine tofauti.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Uefa, vikosi hivyo ambavyo ni Barcelona, Juventus na Real Madrid havitapigwa marufuku ya kunogesha soka ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) jinsi ilivyopendekezwa awali.

Arsenal, Liverpool, Chelsea, Manchester City, Tottenham Hotspur na Manchester United kutoka Uingereza; Atletico Madrid ya Uhispania pamoja na AC Milan na Inter Milan za Italia zilijiondoa kwenye mpango huo wa kujiunga na ESL saa chache baada ya kushutumiwa na mashabiki.

Vikosi 12 vya soka ya bara Ulaya vilikutana Aprili 2021 na kutangaza mpango wa kuunda kipute kipya cha ESL ambacho kingechukua mahali pa UEFA.

 Benki ya JP Morgan Chase kutoka Amerika ilitarajiwa kuwa mfadhili wa kivumbi hicho cha ESL. Waasisi wa mpango huo wa kuzindua ESL walijaribu pia kushawishi klabu za Bayern Munich na Paris Saint-Germain (PSG) za Ujerumani na Ufaransa mtawalia bila mafanikio.

Vikosi vya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) vilikuwa vya kwanza kujiondoa kwenye mpango wa kujiunga na ESL kabla ya kufutwa na vile vya Italia (Serie A) kisha Atletico Madrid inayonolewa na kocha Diego Simeone katika Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga).

  • Tags

You can share this post!

Tukipunguza bei ya mafuta tutalemewa kufadhili shughuli za...

Alexander-Arnold na Maguire kutochezea Uingereza dhidi ya...