Uhispania kutua Ugiriki leo vita vya Qatar 2022

Uhispania kutua Ugiriki leo vita vya Qatar 2022

ATHENS UGIRIKI

Na MASHIRIKA

Ugiriki watakuwa nyumbani leo usiku kualika Uhispania katika mechi Kundi B ya mchujo wa kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia za mwaka ujao.

Wenyeji wanarejea uwanjani baada ya kuchapwa 2-0 na Uswidi (Sweden) katika mechi yao ya mwisho kundini humo, kikiwa kichapo cha kwanza kutoka kwa Ugiriki ambao hapo walitoka sare mara tatu na kushinda mbili.

Kwa upande mwingine, Uhispania wamerejea baada ya kuandikisha ushindi dhidi ya Georgio na Kosovo mtawaliwa. Waliandikisha ushindi huo kwa wapinzani wao nyumbani na ugenini, lakini wakashindwa 2-1 na Sweden.

Uhispania wanashikilia nafasi ya pili kwenye Kundi hilo la B wakiwa na pointi 13 kutokana na mechi sita. Wanahitaji pointi moja katika mechi ya leo ili kutinga hatua ya mchujo, lakini ushindi utawawezesha kuwapiku Sweden na kutwaa uongozi wa kundi hilo.

Kwingineko, Ureno watakuwa ugenini kukabiliana na wenyeji Ireland ya kocha Stephen Kenny katika pambano la Kundi A linalotarajiwa kuwa ngumu kwa timu zote mbili, wakati Ujerumani ambao tayari wamefuzu wakisubiri nyumbani kuvaana na limbukeni Liechtenstein katika mechi ya Kundi J.

Mechi hiyo itachezewa Volkswagen Arena.Wakati huo huo, nahodha Gareth Bale yuko katika hali nzuri ya kuchezea nchi yake kwa mara ya 100, hii ni kulingana na mwenzake Wayne Hennesssey.Mshambuliaji huyo wa Real Madrid hajachezea Wales tangu aumie mwezi Septemba, lakini amerejea mazoeini akiwa tayari kucheza Jumamosi dhidi ya Belarus kwenye mechi nyingine ya michuano hiyo itakayochezewa Cardiff City.

Iwapo atapewa nafasi kikosini siku huyo Bale, mwenye umri wa miaka 32 atakuwa raia wa pili wa taifa hilo kuchezea timu ya taifa mara 100 baada ya mustaafu Chris Gunter.“Kwa hakika ameonyesha kiwango kizuri mazoezini na huenda mchango wake ukasaidia timu kwa kiasi kikubwa,” aliongeza kipa Hennessey.

“Yuko katika kiwango kizuri, ana tabasamu na kucheka kila wakati- na kawaida anapokuwa kikosini mambo huwa safi,” aliongeza mlinda lango huyo wa klabu ya Burnley.Kiungo Joe Allen aliongeza: Kila mara anapojiandaa, anaonekana kuwa katika hali njema. Ni mchezaji muhimu wa kutegemewa na kwa hakika yuko tayari.

Nataraji atacheza Jumamosi kusaidia timu katika mechi hii muhimu.”Jeraha la Bale lilimweka nje katika mechi za kufuzu za Oktoba na hajachezea Madrid tangu Agosti 28.Mara yake ya mwisho kuchezea timu ya taifa ilikuwa Septemba Wales ilipokabiliana na Estonia katika mechi iliyomalizika kwa sare ya 0-0.

Alipoulizwa iwapo kukaa kwake nje kwa mwezi mzima kutavuruga kiwango chake, Hennessey alisema tayari nyota huyo yuko katika hali nzuri ya kung’ara.Hennessey ambaye anajivunia rekodi ya mechi 97 na Bale wamekuwa marafiki wa karibu kwa miaka mingi, baada ya kucheza pamoja katika timu ya taifa ya vijana.

Wales na Jamhuri ya Czech wanatoshana na kwa pointi katika Kundi E, lakini Wales wamecheza. Baada ya kumalizana na Belarus, watakaribisha vinara wa kundi hilo Ubelgiji Jumanne ijayo. Ratiba ya Leo: Azerbaijan na Luxembourg, Armenia na Macedonia Kaskazini, Urusi na Cyprus, Georgio na Sweden, Slovakia na Slavenia, Romania na Iceland, Ujerumani na Leichtenstein, Malta na Croatia, Ugiriki na Uhispania, Ireland na Ureno.

You can share this post!

Ferdinand apendekeza Ole Gunnar atimuliwe

Kongamano la ugatuzi ni kwa waliochanjwapekee -Waandalizi

T L