Uhispania wakabwa koo na Ugiriki

Uhispania wakabwa koo na Ugiriki

Na MASHIRIKA

UHISPANIA walijikwaa katika mechi yao ya kwanza ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia baada ya kulazimishiwa sare ya 1-1 na Ugiriki mjini Granada mnamo Alhamisi.

Alvaro Morata aliwapa Uhispania bao la kwanza katika dakika ya 33, sekunde chache baada ya Dani Olmo kushuhudia fataki yake ikizuiliwa na mwamba wa goli la Ugiriki.

Inigo Martinez aliyeletwa uwanjani katika kipindi cha pili alimchezea visivyo kiungo Giorgos Masouras wa Ugiriki na kuchangia penalti iliyojazwa kimiani na Anastasios Bakasetas katika dakika ya 56.

Licha ya washambuliaji wa Uhispania kukita kambi langoni mwa Ugiriki kwa muda mrefu katika kipindi cha pili, masogora wa kocha Luis Enrique walipoteza nafasi nyingi za wazi na wakalazimika kuridhika na alama moja pekee.

Morata ambaye kwa sasa anachezea Juventus ya Italia kwa mkopo kutoka Atletico Madrid ya Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga), alikuwa na nafasi maridhawa ya kufungia timu yake goli la ushindi ila akazidiwa maarifa na kipa wa Ugiriki.

Uhispania kwa sasa wanajiandaa kwa mechi itakayowakutanisha na Georgia mnamo Machi 28, siku ambapo Ugiriki nao watakuwa wenyeji wa Honduras.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Ujerumani yakomoa Iceland 3-0

Uhuru asukuma Ruto, Raila kona moja