Uhispania wakomoa Ureno ugenini na kutinga nusu-fainali za Uefa Nations League

Uhispania wakomoa Ureno ugenini na kutinga nusu-fainali za Uefa Nations League

Na MASHIRIKA

ALVARO Morata alifunga bao la pekee na la ushindi dhidi ya Ureno mnamo Jumanne usiku jijini Braga na kusaidia timu yake ya taifa ya Uhispania kutinga nusu-fainali za Uefa Nations League.

Nyota huyo wa zamani wa Chelsea alicheka na nyavu za wenyeji wao katika dakika ya 88 baada ya kuandaliwa krosi safi na Nico Williams.

Ureno walishuka dimbani wakihitaji alama moja pekee ili kufuzu kwa nusu-fainali ambayo ingeweka hai matumaini yao ya kunyanyua taji la Nations League kwa mara ya pili baada ya kukomoa Uholanzi 1-0 mnamo 2019 jijini Porto.

Hata hivyo, walipoteza nafasi nyingi za wazi kupitia kwa fowadi Diogo Jota wa Liverpool na mvamizi matata wa Manchester United, Cristiano Ronaldo.

Uhispania sasa wanaungana na Croatia, Italia na Uholanzi kwenye hatua ya nne-bora ya kipute cha Nations League itakayoandaliwa jijini Amsterdam kati ya Juni 14-18, 2023.

Uhispania walikuwa wanafainali ya Nations League mnamo 2021 na wakazidiwa ujanja na Ufaransa kwa mabao 2-1 katika uwanja wa San Siro jijini Milan, Italia.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

ZARAA: Wajukuu wanafurahia matunda ya bidii yake

Mshukiwa wa wizi wa vyuma vilivyoibwa kutoka Industrial...

T L