Uhispania wapewa Italia huku Uholanzi wakionana na Croatia kwenye nusu-fainali za Uefa Nations League

Uhispania wapewa Italia huku Uholanzi wakionana na Croatia kwenye nusu-fainali za Uefa Nations League

Na MASHIRIKA

UHISPANIA watakutana na Italia kwenye nusu-fainali za kipute cha Uefa Nations League mwaka huu huku wenyeji Uholanzi wakipepetana na Croatia.

Mechi hizo za hatua ya nne-bora zimeratibiwa kusakatwa kati ya Juni 14-15 huku fainali na mechi nyingine ya  kutafuta mshindi nambari tatu na nne ikitandazwa Juni 18. Michuano yote itapigiwa mjini Rotterdam au Enschede.

Uhispania walitandika Italia 2-1 katika nusu-fainali za Nations League mnamo 2021 kabla ya kuzidiwa ujanja na Ufaransa kwa kichapo cha 2-1 kwenye fainali.

Uholanzi nao walitandikwa 1-0 na wenyeji Ureno katika fainali ya kipute hicho mnamo 2019.

DROO YA NUSU-FAINALI ZA NATIONS LEAGUE:

Uholanzi vs Croatia, Juni 14, De Kuip, Rotterdam

Uhispania vs Italia, 15 June, uga wa FC Twente, Enschede

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Fahamu tano bora za KWPL

MASHEMEJI: AFC Leopards kualika Gor Mahia ugani Nyayo mnamo...

T L