Uhuru aomba msamaha kutoka kwa waliokerwa na utawala wake

Uhuru aomba msamaha kutoka kwa waliokerwa na utawala wake

NA WANDERI KAMAU

RAIS Uhuru Kenyatta Jumapili aliomba msamaha kwa Wakenya wanaohisi aliwakosea kwa zaidi ya miaka tisa aliohudumu kama rais.

Rais Kenyatta pia aliomba msamaha kwa ahadi ambazo huenda alikosa kuwatimizia Wakenya.

Kwenye mahojiano ya pamoja na vituo vya redio na runinga vinavyotangaza katika eneo la Mlima Kenya, Rais alisema kuwa alitekeleza majukumu yake kulingana na uwezo aliokuwa nao.

“Huenda kuna watu niliowakosea bila kukusudia kwa muda niliokuwa uongozini. Ninawaomba msamaha, kwani mimi pia ni binadamu. Niwieni radhi, kwani nilifanya niliyoweza. Binafsi, pia nina mapungufu yangu,” akasema Rais Kenyatta.

Rais Kenyatta amekuwa akilaumiwa na baadhi ya Wakenya, hasa washirika wa Naibu Rais William Ruto kwa “kumsaliti kisiasa” licha yake kumsaidia pakubwa kushinda urais kwenye chaguzi za 2013 na 2017.

Hata hivyo, Rais Kenyatta amekuwa akisisitiza kuwa Dkt Ruto na washirika wake ndiyo wamekuwa chanzo kikuu cha kusambaratika kwa baadhi ya mipango aliyokuwa nayo.

  • Tags

You can share this post!

Hofu baadhi ya karatasi za kura zikikosekana

Gachagua aahidi wakazi ushindi mkuu

T L