Uingereza wakomoa Italia na kufuzu kwa fainali ya Euro U-19 itakayowakutanisha na Israel

Uingereza wakomoa Italia na kufuzu kwa fainali ya Euro U-19 itakayowakutanisha na Israel

Na MASHIRIKA

UINGEREZA walitinga fainali ya Euro kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 19 mwaka huu baada ya kutoka nyuma na kukomoa Italia 2-1 katika nusu-fainali mnamo Jumanne usiku nchini Slovakia.

Matineja wa Uingereza walijipata chini katika dakika 12 baada ya Fabio Miretti kuwaweka Italia uongozini kupitia penalti iliyotokana na tukio la Brooke Norton-Cuffy kumchezea sogora huyo wa Juventus visivyo ndani ya kijisanduku.

Hata hivyo, Alex Scott alitokea benchi na kusawazishia Uingereza katika dakika ya 58 kabla ya beki wa Liverpool, Jarell Quansah kufunga bao la ushindi mwishoni mwa kipindi cha pili.

Uingereza sasa watavaana na Israel kwenye fainali baada ya kikosi hicho kuduwaza Ufaransa kwa mabao 2-1 kwenye nusu-fainali ya pili.

Uingereza wanaonolewa na kocha Ian Foster, watashuka dimbani kwa ajili ya fainali wakipania kuendeleza ubabe uliowavunia ushindi wa 1-0 dhidi ya Israel katika mojawapo ya mechi za makundi ya Euro 2022.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Shirika la feri lakubali lawama kuhusu ajali

Arama asukumwa jela miezi sita

T L