Uingereza wapewa Ireland ya Kaskazini kwenye mchujo wa kufuzu Kombe la Dunia 2023

Uingereza wapewa Ireland ya Kaskazini kwenye mchujo wa kufuzu Kombe la Dunia 2023

Na MASHIRIKA

TIMU ya taifa ya Uingereza itakutana na Northern Ireland kwenye Kundi D baada ya kutiwa katika zizi moja la mechi za kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia la Wanawake zitakazoandaliwa kwa pamoja na mataifa ya Australia na New Zealand mnamo 2023.

Scotland ambao walifuzu kwa fainali hizo kwa mara ya kwanza mnamo 2019, wamepangwa kuvaana na Uhispania na Ukraine kwenye Kundi B.

Wales wamo katika zizi moja la Kundi I kwa pamoja na wenyeji wa fainali za mwaka wa 2019, Ufaransa.

Uingereza na Northern Ireland walioweka historia kwa kufuzu kwa fainali za Euro 2022, pia watakabiliana na Austria, North Macedonia, Latvia na Luxembourg.

Jamhuri ya Ireland wametiwa katika Kundi A kwa pamoja na Uswidi waliowapiga Uingereza mnamo 2019 na kuambulia nafasi ya tatu.

Fainali hizo zitaleta pamoja jumla ya mataifa 51 huku mechi zikipigwa kati ya Septemba 2021 na Septemba 2022.

Mechi za hatua ya 32-bora zimeratibiwa kusakatwa kati ya Julai na Agosti 2023 baada ya ushiriki wa kivumbi hicho kupanuliwa kutoka timu 24 hadi 32 mnamo 2019.

Washindi wa makundi tisa ya kufuzu watajikatia tiketi za moja kwa moja za fainali huku nambari mbili wakifuzu kwa mchujo utakaofanyika mnamo Oktoba 2022.

DROO:

Kundi A: Sweden, Finland, Jamhuri ya Ireland, Slovakia, Georgia

Kundi B: Spain, Scotland, Ukraine, Hungary, Faroe Islands

Kundi C: Uholanzi, Iceland, Jamhuri ya Czech, Belarus, Cyprus

Kundi D: Uingereza, Austria, Northern Ireland, North Macedonia, Latvia, Luxembourg

Kundi E: Denmark, Urusi, Bosnia-Herzegovina, Azerbaijan, Malta, Montenegro

Kundi F: Norway, Ubelgiji, Poland, Albania, Kosovo, Armenia

Kundi G: Italia, Uswisi, Romania, Croatia, Moldova, Lithuania

Kundi H: Ujerumani, Ureno, Serbia, Israel, Uturuki, Bulgaria

Kundi I: Ufaransa, Wales, Slovenia, Greece, Kazakhstan, Estonia

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

RB Leipzig wachabanga Werder Bremen na kutinga fainali ya...

NASAHA: Ni muhimu kwa muumini kudumu katika kuomba msamaha