Uingereza yaahidi kupiga jeki uchumi wa Kenya

Uingereza yaahidi kupiga jeki uchumi wa Kenya

Na MARY WANGARI

SERIKALI YA UINGEREZA imeelezea nia yake ya kushirikiana na Kenya kufufua mifumo ya uchumi nchini kufuatia athari za Covid-19.

Serikali hiyo pua itaharakisha hatua za kudhibiti mabadiliko ya hali ya anga kupitia kongamano la kimataifa linaloendelea la COP26. Akihutubia vyombo vya habari jana katika hafla iliyoandaliwa Muthaiga Country Club, Nairobi, Mbunge wa Uingereza anayesimamia Biashara Kenya, Theo Clarke, alisema Uingereza imejitolea kushirikiana na Kenya kupiga vita ufisadi.

Aidha, aliipongeza Kenya kwa juhudi zake za kukabiliana na athari hasi za mabadiliko ya hali ya anga akirejelea Kongamano la Kitaifa lililoanza Jumapili na linalotazamiwa kukamilika hii leo (Ijumaa).

“Serikali ya Kenya imejitolea kushirikiana na Kenya kukomesha ufisadi hasa kuambatana na ripoti iliyotolewa na Tume ya Kitaifa kuhusu Maadili na Kukabiliana na Ufisadi Kenya (EACC) mnamo 2015,”“Tumeridhishwa na juhudi za Kenya katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya anga hasa wakati huu mataifa ya dunia yamejumuika katika Kongamano la Awamu ya 26 kujadiliana kuhusu mwelekeo wa kukabili Mabadiliko ya hali ya Anga, COP26,” alisema Bi Clarke.

You can share this post!

JUMA NAMLOLA: Bunge lisitumiwe kama ‘danganya...

Wanjigi aelezea imani atambwaga Raila na kubeba bendera ODM

T L