UJAUZITO NA UZAZI: Tatizo la ‘lochia’ baada ya kujifungua

UJAUZITO NA UZAZI: Tatizo la ‘lochia’ baada ya kujifungua

NA PAULINE ONGAJI

AKINA mama wengi hukumbwa na tatizo la kuendelea kuvuja damu kutoka ukeni miezi kadhaa baada ya kujifungua.

Shida hii inafahamika kama Lochia kwa lugha ya kitaalamu, na hutegemea na upesi wa mwili kuondoa uchafu kama uchafu kama kamasi, mabaki ya mji na damu baada ya kujifungua.

Lochia, huwa sawa na kuvuja damu kunaotokea wakati wa hedhi, lakini wakati huu damu hii hua nyingi sana. Huanza saa kadha baada ya kujifungua na huendelea kwa muda wa kati ya wiki mbili na tatu. Lakini kwa wanawake wengine, shida hii hudumu kwa hata wiki sita.

Ishara za Lochia

· Kutokwa na damu nyingi kutoka sehemu ya uke, inayoambatana na migando ya damu kwa zaidi ya siku saba baada ya kujifungua

·Kutokwa na majimaji yanayotoa harufu mbaya

·Homa na kuashwa

·Kisunzi, kuumwa na kichwa na uchovu

· Kuvuja damu kuliko kwa kawaida(ambapo kisodo kizito kinalowa chini ya saa moja)

Ni nini kinachosababisha hali hii?

Kwa mara nyingi hali hii hutokea wakati chupa ya uzazi inapokosa kurejea hali yake ya kawaida baada ya kujifungua. Hii husababisha sehemu hii kuendelea kuvuja. Mambo mengine yanayosababisha hali hii ni pamoja na:

· Kukosa kuondoka kwa mji wote baada ya kujifungua

· Kutolewa kwa mji kwa nguvu

· Majeraha kwa chupa ya uzazi, njia ya uzazi au uke wakati wa kujifungua

Jinsi ya kukabiliana na hali hii

· Pumzika sana huku ukiepuka kusimama na kutembea kwingi

· Tumia visodo vizito ili kudhibiti kiwango cha damu kinachotoka

· Usitumie visodo vya kuingiza ukeni kwa wiki sita baada ya kujifungua kwani vyaweza leta bacteria ukeni na hata kusababisha maambukizi

Kila mwanamke yuko katika hatari ya kukumbwa na shida hii, lakini kuna sababu nyingine zinazoongeza uwezekano wa kuathirika.

· Kujifungua zaidi ya mtoto mmoja kwa wakati mmoja

· Placenta previa, hali inayotokea wakati mji unaposhikana na ukuta wa chupa ya uzazi kiwango cha kufunika njia ya uzazi.

Hali hii hutokea sana wakati wa kujifungua mtoto wa pili

· Uchungu wa kuzaa uliochochewa

· Kumzaa mtoto mkubwa

Hali hii hutibiwa vipi?

· Kukandwa katika sehemu ya chupa ya uzazi ili kusisimua misuli na hivyo kupunguza kuvuja kwa damu

· Matumizi ya dawa zinazopunguza kuvuja damu kuambatana na ushauri wa daktari

· Kuoundolewa kwa mji uliyosalia kwa kutumia mkono

· Kuongezewa damu

· Kuondolewa kwa chupa ya uzazi iwapo imeharibika.

  • Tags

You can share this post!

Mtimkaji wa mbio fupi Makena ashinda kilomita 10 mbio za...

Alipanga kifo chake kwa miaka 7

T L