Habari Mseto

Ujenzi wa chuo cha teknolojia Konza kuanza

February 13th, 2019 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Serikali inalenga kuzindua ujenzi wa chuo kikuu katika Jiji la Konza Technopolis.

Hii ni kwa kushirikiana na Serikali ya Korea Kusini kupitia kwa Wizara ya Elimu.

Wizara hiyo imeunda kamati itakayochora majumba na mtalaa wa chuo hicho unaohusisha Korea Advanced Institute of Science and Technology, Architects & Engineering Co. Ltd. Na SUNJIN Engineering & Architecture CO. Ltd.

Chuo hicho kitaitwa Kenya Advanced Institute of Science & Technology (Kenya- KAIST) na kitashirikiana na Korean Advanced Institute of Science & Technology (Korea- KAIST) ambacho kilianzishwa kufanya utafiti wa kisayansi na teknolojia, ambayo inahitajika zaidi nchini.

“Tunataka kuzindua mandhari mema ya wanafunzi kutoka sio tu Kenya lakini pia eneo la Africa Mashariki,” alisema Mwenyekiti wa Mamlaka ya Maendeleo ya Jiji la Konza Reuben Mutiso.

Kulingana naye, taifa lililo na watu wrengi walioelimika hukua haraka kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Ujenzi wa chuo hicho unalenga kutoa wahandisi na wanasayansi wanaoweza kufanya utafiti kulifaa taifa la Kenya.