Habari MsetoSiasa

Ukabila umepitwa na wakati, tupendane – Lonyangapuo

June 4th, 2019 1 min read

Na PETER MBURU

GAVANA wa West Pokot John Lonyangapuo amerejea vinywani mwa watu tena, kufatia wito wake mpya kwa wakazi wa kaunti yake, anapolenga kuhakikisha kuwa hawatengani wala kuwa na chuki.

Gavana Lonyangapuo akihutubia umma aliwataka wakazi wa kaunti yake kupendana bila kujali kabila ama wanasiasa wanaounga mkono, akiwaambia ni mandugu.

Lakini wito wake kuwa walambane ndio umewaacha wengi na vicheko, wakishangaa ikiwa gavana huyo alimaanisha kulambana halisi.

“Nataka niwaombe kwamba, haijalishi wewe ni kabila gani kwanza ukiwa hapa West Pokot. Nataka mlambane na mpendane na jirani yako,” akasema Profesa Lonyangapuo.

Aliendelea kuwaambia “Haijalishi wewe ni wa chama gani, kama KANU kama mimi, wengine Jubilee, ati sahii bado mnaringa na hivyo vitu, viliisha. Kwa sasa tupendane.”