Makala

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Ufundishaji wa lugha kimawasiliano

June 6th, 2019 1 min read

Na MARY WANGARI

NI muhimu kuhakikisha kwamba katika kujifunza lugha shughuli ya ufundishaji inayotumika ni mawasiliano.

Vilevile, ni sharti kuwepo na matumizi ya mbinu mwafaka za kufundisha lugha ngeni na lugha ya pili.

Jambo lingine muhimu la kuzingatia katika ufundishaji na ujifunzaji wa lugha ni kwamba mchakato huu husisitiza mwingiliano – maathiriano kama mbinu ya kujifunza lugha.

Kazi za lugha

Kwa mujibu wa Van (1975), lugha inatekeleza kazi zifuatazo katika jamii:

i. Kutoa habari.

ii. Kusimulia.

iii. Kuuliza.

iv. Kutoa taarifa.

v. Kutafuta taarifa za kitaaluma.

vi. Kuelezea mihemko na misisimko.

vii. Kuelezea masuala ya uadilifu. Kwa mfano, kuomba msamaha, ibada na kadhalika.

viii. Kwenye mambo ya ushirikiano katika jamii. Mfano, kuamkua watu, kujitambulisha na kadhalika.

Ni muhimu kukumbuka kwamba hata ikiwa mwanafunzi ana malengo mengine ya kujifunza lugha husika, ni sharti mwalimu amfundishe umuhimu wa lugha hiyo kulingana na muktadha.

 

[email protected]

Marejeo

Massamba, D.P.B. (2002). Historia ya Kiswahili 50 BK. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

Ipara, I. O. & Waititu, F.G. (2006). Ijaribu na Uikarabati. Nairobi: Oxford University Press.

Habwe, J. (2006). Darubini ya Kiswahili, Nairobi: Phoenix Publishers.

Maddo, U. & Thiong’o, D. (2006). Mazoezi na Udurusu: Kiswahili 102/2. Nairobi, Global Publisher.