Makala

ULIMBWENDE: Jinsi unavyoweza kuondoa mwenyewe kucha bandia

September 25th, 2019 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

KWENDA saluni kubandikwa kucha ni rahisi sana lakini watu wengi hawapendi pale zinapoanza kupoteza mvuto na inabidi urudi tena saluni kuzitoa.

Wengi huwa wanachagua kukaa nazo hivvo – nusu zipo, nusu hazipo – kisa tu uvivu au kuwa na mambo mengi na huna nafasi ya kwenda saluni kuzitoa.

Basi usihofu kwa sababu unaweza kubandua au kuondoa kucha bandia mwenyewe nyumbani.

Unahitaji

  • Acetone
  • Nail clippers
  • Nail buffer au tupa yaani file
  • pamba
  • Aluminum foils
  • Mafuta ya lanolin

Namna ya kufanya

Kata kucha ziwe fupi.

Ondoa rangi kwa kutumia Nail buffer au file.

Paka mafuta ya lanolin katika ngozi pembeni mwa kucha zako kisha chukua pamba na uingize katika acetone na kisha weka kwa kucha zako.

Kata kipande cha aluminium foil na ufunge ukucha wako ambao umeweka pamba ili pamba isianguke.

Subiri kwa dakika baina ya 25-30.

Ondoa aluminium foil yako; inatakiwa ukucha bandia utoke nayo. Kama si hivyo, funga tena, acha kwa muda kisha ujaribu tena kutoa.

Namna ya pili

Unaweza kuondoa kucha bandia kwa maji fufutende.

Mahitaji

  • maji
  • acetone
  • bakuli mbili

Namna ya kufanya

Chemsha maji fufutende kisha mimina kwenye bakuli.

Chukua bakuli jingine, ingiza katika bakuli la maji ya uvuguvugu na umiminie acetone.

Ingiza vidole vyako na uviache kwa muda katika bakuli lenye acetone, kucha zikisha legea unaweza kuanza kuzitoa.