Makala

ULIMBWENDE: Jinsi ya kuondoa uchafu kwenye ngozi ukitumia scrub ya kahawa

September 11th, 2019 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

KUNAKUWA na uchafu kwenye ngozi hata baada ya kuoga.

Scrub nzuri ya kuondoa weusi huo ni sukari na mafuta ya mizeituni ambayo inapakwa kisha unafanyia masaji mwili mzima kuondoa uchafu wa ngozi.

Jinsi ya kuandaa

  • chukua kahawa vijiko viwili
  • kijiko kimoja cha sukari
  • mafuta ya mizeituni vijiko vinne

Changanya vyote kwa pamoja upate mchanganyiko.

Baada ya hapo, chukua mchanganyiko huo, paka mwilini mwako, ufanyie mwili masaji kama unayesugua; hasa sehemu nyeusi. Shughuli hiyo ifanye wakati unaoga.

Sehemu nyeusi kama kwenye maungio, makwapani na shingoni, hizi ni sehemu ambazo weusi wake huwa unazidi hivyo kwa kutumia mchanganyiko huu unaweza kurudisha rangi asili ya ngozi yako.

Kwa wanaotaka kung’arisha miguu scrub hii pia ni nzuri.

Vile vile Kahawa ina matumizi mengine Kama kuondoa michirizi na chunusi

Scrub ya kahawa kwa michirizi.

Chukua kahawa na mafuta ya nazi, changanya vizuri kisha itumie kama scrub sehemu ambapo una michirizi.

Scrub polepole kwa robo saa kisha oga kwa maji ya ufufutende.

Kausha na upake losheni.

Scrub ya kawaha kuondoa chunusi.

Vitu unavyohitaji ni kahawa, mafuta ya nazi na mdalasini.

Changanya vizuri kiasi sawa kwa kila kitu.

Paka usoni na uwe kama unasugua polepole kwa muda wa dakika 10.

Nawa uso kwa maji ya ufufutende kisha paka moisturizer.

Fanya hivi mara mbili kwa wiki. Utaona matokeo mazuri.